Misale Ya Waomini

In this video, we will learn at how to install IBM DB2 Express-C and Data Studio. Once installed, we log into the db2inst1 user account and begin the setup. Install centos 7 with gui.

• • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • > > 6/10/2011 8:27:54 AM Misale Mpya ya Waamini kwa lugha ya Kiingereza ni utajiri mkubwa katika maadhimisho ya Liturjia ya Kanisa Baraza la Maaskofu Katoliki Uingereza linasema, tafsiri mpya ya Misale ya Waamini kwa lugha ya Kiingereza, dhamana iliyotekelezwa kwa kuwahusisha Maaskofu mia saba kutoka sehemu mbali mbali za dunia, itakuwa ni msaada mkubwa kwa ajili ya watumiaji wa lugha ya Kiingereza. Mabadiliko yaliyofanywa ni kuhakikisha kwamba, Maaskofu wanakuwa waaminifu kwa Mapokeo ya Liturjia ya Kanisa kwa kuzingatia machapisho halisi mintarafu Maandiko Matakatifu.

Maaskofu wanasema, kuna uhusiano mkubwa kati ya Liturjia na Neno la Mungu, kwani Neno la Mungu linamwilishwa katika maadhimisho ya Liturjia ya Kanisa. Kwa njia hii, Maaskofu wamejitahidi kuhakikisha kwamba, misamiati inayotumika inawasaidia waamini kufahamu kile ambacho Mama Kanisa anaadhimisha kila wakati. Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, wakati alipokuwa anahitimisha hija yake ya kichungaji nchini Uingereza, Septemba, 2010, aliwahimiza Maaskofu wa Uingereza kuhakikisha kwamba, wanatumia fursa ya tafsiri mpya ya Misale ya Waamini kwa Lugha ya Kiingereza kwa ajili ya kufanya katekesi ya kina kuhusu Fumbo la Ekaristi Takatifu na Ibada mbali mbali zinazoadhimishwa na Mama Kanisa.

Waomini

Misale ya Waamini ni kielelezo cha umoja wa Kanisa na chombo makini ambacho Mwenyezi Mungu anapenda kukitumia kwa ajili ya kuwakirimia waja wake neema na baraka wanapoadhimisha Mafumbo ya Kanisa. Kwa mara ya kwanza Misale Mpya ya waamini inatarajiwa kuanza kutumika Jumapili ya kwanza ya Kipindi cha Majilio, kwa mwaka 2011. Kuanzia Mwezi Septemba, hadi Desemba, waamini watatumia Misale hii kwa majaribio, ili kuzoea tafsiri hii mpya ya Misale ya Waamini, hasa mabadiliko yaliyofanywa. Kipindi hiki chote, waamini watasaidiwa kwa njia ya Katekesi ya kina kuhusu Maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu na Tafsiri Mpya ya Misale ya Waamini kwa lugha ya Kiingereza. All the contents on this site are copyrighted ©.

MISALE YA WAUMINI UK 407 Mutashambla Respiqusi Thadeo J4 13 Sept 2005 DSM.